Ripoti mpya iliyotolewa leo inaonyesha kuwa, miaka 10 tangu kusainiwa kwa mkataba wa Paris, serikali nyingi bado zinapanga kuzalisha mafuta ya kisukuku (makaa, mafuta na gesi) kwa kiwango kikubwa zaidi ya inavyokubaliana na malengo ya kudhibiti ongezeko la joto duniani. Ifikapo mwaka 2030, uzalishaji uliopangwa utakuwa zaidi ya mara mbili (asilimia 120) ya kiwango kinachohitajika ili dunia ibaki ndani ya 1.5°C, na asilimia 77 zaidi ya lengo la 2°C.
Hali hii inamaanisha kwamba dunia itazidi kuenda mbali na malengo ya mkataba wa Paris, hata wakati nchi zinawasilisha ahadi mpya za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuondokana na mafuta ya kisukuku. Tathmini ya mwisho ya mwaka 2023 ilionyesha pengo la uzalishaji wa mafuta ya kisukuku kuwa asilimia 110 zaidi ya ratiba ya 1.5°C, na asilimia 69 zaidi ya ratiba ya 2°C.
Mambo muhimu kutoka Ripoti ya Production Gap ya 2025:
Ripoti hii imetolewa na taasisi tatu: Stockholm Environment Institute (SEI), Climate Analytics, na International Institute for Sustainable Development (IISD). Ripoti hii Inachambua mipango ya serikali kuhusu uzalishaji wa makaa ya mawe, mafuta, na gesi dhidi ya viwango vinavyolingana na kudhibiti ongezeko la joto duniani hadi 1.5°C au 2°C.
“Mwaka 2023, serikali zilikubali rasmi haja ya kuachana na mafuta ya kisukuku ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi – jambo ambalo Mahakama ya Kimataifa ya Haki sasa imesisitiza,” asema Derik Broekhoff, mwandishi mkuu wa ripoti na Mkurugenzi wa Programu ya Sera za Tabianchi katika SEI Marekani. “Lakini ripoti yetu inaonyesha wazi kuwa, ingawa baadhi ya nchi zimejitolea kwa mpito wa nishati safi, nyingi bado zinatumia mkakati wa zamani unaotegemea mafuta ya kisukuku.”
Uchambuzi wa ripoti ya 2025 umejikita kwenye nchi 20 zinazozalisha karibu asilimia 80 ya mafuta ya kisukuku duniani, ikiwemo Australia, Brazil, Kanada, China, India, Nigeria, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Uingereza, na Marekani. Ripoti inabainisha kuwa nchi 17 kati ya 20 bado zinapanga kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kisukuku kufikia mwaka 2030. Nchi 11 kati ya hizo sasa zinatarajia viwango vya juu zaidi vya uzalishaji kuliko walivyopanga mwaka 2023. Hata hivyo, idadi ya nchi zinazolingana mipango yao na mpito kuelekea sifuri halisi ya hewa chafu imeongezeka kutoka nne mwaka 2023 hadi sita mwaka huu.
“Ili kufikia lengo la 1.5°C, dunia inahitaji kupunguza kwa haraka uwekezaji katika makaa ya mawe, mafuta, na gesi, na kuelekeza rasilimali hizo kwenye mpito wa nishati safi unaozingatia usawa na haki,” asema Emily Ghosh, mwandishi mwenza wa ripoti na Mkurugenzi wa Programu ya Mpito wa Haki katika SEI Marekani. “Kufikia COP30, serikali lazima zijitolee kuongeza nishati mbadala, kuondoa mafuta ya kisukuku, kudhibiti mahitaji ya nishati, na kutekeleza mabadiliko ya nishati yanayoongozwa na jamii.”
Zaidi ya watafiti 50 kutoka kote duniani walishiriki katika uchambuzi na mapitio ya ripoti hii, wakitoka katika vyuo vikuu, taasisi za utafiti, na mashirika ya kimataifa
Ripoti hii iwe onyo na mwongozo. Nishati mbadala hatimaye itachukua nafasi ya mafuta ya kisukuku, lakini tunahitaji hatua madhubuti sasa ili kufunga pengo kwa wakati.”
– Christiana Figueres, Katibu Mkuu wa zamani wa UNFCCC
“Kuongezeka kwa mipango ya upanuzi wa mafuta ya kisukuku katika miaka miwili iliyopita ni jambo la kutisha. Serikali nyingi zinaona nishati mbadala kama suluhisho la usalama wa nishati, lakini nyingine bado zinapinga mpito huu safi.”
– Olivier Bois von Kursk, mwandishi mwenza wa ripoti na mshauri wa sera katika IISD
“Miaka kumi baada ya Paris, nishati mbadala iko mbele sana. Badala ya kujiunga na mbio, serikali nyingi zinaejea nyuma kwa sera za zamani. Kutumia pesa za umma kwa miradi itakayokuwa mali iliyokwama ni hasara na dhuluma kubwa kwa binadamu na mazingira.”
– Neil Grant, mwandishi mwenza wa ripoti na mtaalamu mwandamizi katika Climate Analytics
Ulrika Lamberth, Simu: +46 73 801 7053, Afisa Habari Mwandamizi, SEI (Stockholm, Uswidi),na Lynsi Burton, Simu: +1 360 485 3041, Afisa Mawasiliano, SEI (Seattle, Marekani)
Paul May, Mkuu wa Mawasiliano, Climate Analytics (Berlin, Ujerumani), na Neil Grant, Mchambuzi wa Nishati na Tabianchi, Climate Analytics (Berlin, Ujerumani)
Megan Darby, Afisa Mwandamizi wa Mawasiliano, IISD (London, Uingereza), na Aia Brnic, Afisa Mwandamizi wa Mawasiliano, IISD (Geneva, Uswisi)
Other publication / Governments, in aggregate, still plan to produce far more fossil fuels than would be consistent with limiting global warming to between 1.5ºC and 2ºC.
SEI, IISD and Climate Analytics.



